1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Obama alihutubia bunge kwa mara ya kwanza.

Abdu Said Mtullya25 Februari 2009

Rais Barack Obama leo amelihutubia bunge la nchi yake kwa mara ya kwanza tokea aingie madarakani.

https://p.dw.com/p/H0ij

WASHINGTON.

Rais Barack Obama  amesema  utawala wake unaanzisha enzi mpya ya kidiplomasia ya kujizatiti katika kuleta amani Mashariki ya Kati ,sambamba  na kuendeleza harakati  za kupambana  na ugaidi.

Rais Obama  amesema hayo leo  katika hotuba yake muhimu ya kwanza bungeni,  tokea aingie madarakani.

Rais huyo pia ameahidi kuimarisha mifungamano  iliyopo na kuanzisha mipya duniani  kote.

Katika hotuba  yake Obama pia amesisitiza umuhimu wa mazungumzo ili kuondoa tofauti.

Juu ya mgogoro wa kiuchumi rais huyo wa  43  wa Marekani  ameahidi kushirikiana  na  nchi zingine zenye nguvu kubwa   za kiuchumi ili kuepusha uwezekano wa kuenea  kwa sera  za kujenga vizingiti vya  kibiashara duniani.

Katika kufikia lengo hilo Marekani itakuwa pamoja na nchi za G 20  ili kurejesha  imani katika mfumo wa fedha na  kuhamasisha utashi wa  bidhaa za Marekani kwenye masoko  ya dunia.

DPAE.