1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Obama asisitiza umuhimu wa mawasiliano baina ya waislamu na nchi za magharibi

Abdu Said Mtullya10 Novemba 2010

Rais Obama atoa mwito mwingine wa kuleta uhusiano mzuri baina ya nchi za kiislamu na za magharibi.

https://p.dw.com/p/Q3Tr
Rais Barack Obama na mkewe Michelle wakiwasili Indonesia kuanza ziara.Picha: AP

JAKARTA:

Rais Obama ameishutumu vikali mipango ya Israel ya kuendelea na ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi mashariki mwa Jerusalem, sehemu ya waarabu.

Rais Obama amesema mipango hiyo haisaidii.

Akizungumza katika ziara ya nchini Indonesia raisi huyo wa Marekani ameeleza kuwa hatua ya Israel ya kuendelea na ujenzi itayaathiri mazungumzo na wapalestina, ambayo tayari yanayumba.

Rais Obama ametumia fursa ya ziara yake nchini Indonesia, kwa mara nyingine kutoa mwito wa kuleta uhusiano mzuri baina ya nchi za kiislamu na za magharibi.

Baada ya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Susilo Bambang Yudhoyono wa Indonesia Obama amesema kuwa pana haja ya kujenga mawasiliano baina ya Uislamu na nchi za magharibi.

Rais Obama ameondoka Indonesia leo kuelekea Korea ya kusiniambako atahudhuria mkutano wa kilele wa nchi muhimu kiuchumi , za G 20

Mivutano juu ya sera za fedha inatarajiwa kupewa kipaumbele kwenye majadiliano ya viongozi wa nchi hizo yatakayoanza kesho katika mji wa Seoul.