1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin awasihi warusi wampigie kura december pili ijayo

Oummilkheir29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUhx

Moscow:

Mmojawapo wa viongozi wa upande wa upinzani nchini Urusi,bingwa wa zamani wa mchezo wa dama Garry Kasparov amerejea nyumbani baada ya kutumikia kifungo cha siku tano jela.Alikutikana na hatia ya kushiriki katika maandamano yaliyopigwa marufuku mjini Moscow.”Serikali inajitumbukiza katika njia ya hatari inayoweza kuleta uimla” amesema Garry Kaskaporov mbele ya waandishi habari nyumbani kwake mjini Moscow.Wakati huo huo rais Vladimir Putin anawasihi warusi wasimpigie kura yoyote uchaguzi wa bunge utakapoitishwea december pili ijayo.Rais Putin anasema:

“December pili unafqanyika uchaguzi wa baraza la taifa Duma.Kampeni ya uchaguzi unakurubia kumalizika.Mjiito chungu nzima imetolewa wakati wa kampeni hiyo.Kuna porojo pia na ahadi za uongo zilizotolewa.Mie nakwambieni kile ambacho ni muhimu:Kwa hisani zenu msiamini kwamba mkondo wa mambo na uzito wa maendeleo yetu vitasalia kama vilivyo,hiyo ni ndoto ya hatari.Maendeleo yetu tutaweza kwa pamoja kuyaendeleza.Ndio maana december pili ipigieni kura orodha nnayoiongoza ya “Urusi iliyoungana.”