1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Sarkozy wa Ufaransa akamailisha ziara yake nchini Afghanistan

Josephat Charo22 Desemba 2007

Waziri mkuu wa Australia Kelvin Ruud naye amefanya ziara ya kushangaza nchini Afghanistan

https://p.dw.com/p/CfEe
Rais Nicolas Sarkozy wa UfaransaPicha: picture-alliance/dpa

Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, ameondoka nchini Afghanistan kuelekea Tajikistan, baada ya kufanya ziara fupi mjini Kabul.

Kiongozi huyo amekutana na rais wa Afghanistan, Hamid Karzai na baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa wanaohudumu nchini humo wakiwa sehemu ya kikosi cha jumuiya ya kujihami ya kambi ya magharibi, NATO.

Akizungumza baada ya mkutano wake na rais Karzai, rais Sarkozy amesema jumuiya ya kimataifa haipaswi kukubali kushindwa katika vita dhidi ya ugaidi nchini Afghanistan.

Aidha kiongozi huyo ameitolea mwito Pakistan iongeze juhudi za kupambanana na ugaidi katika eneo hilo. Rais Sarkozy ameashiria kwamba Ufaransa huenda iongeze idadi ya wanajeshi wake nchini Afghanistan kusaidia jeshi na polisi.

Wakati huo huo, waziri mkuu wa Australia, Kelvin Ruud, amezuru Afghanistan hii leo katika ziara ambayo haikutangazwa.

Kiongozi huyo amesema Australia itaendelea kuisadia Afghanistan na kuahidi nyongeza ya dola milioni 110 za kimarekani katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Bwana Ruud amekutana na rais Karzai mjini Kabul na kufanya mkutano na waandishi wa habari ulioonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni ya kitaifa.

Kelvin Ruud amewatembelea wanajeshi wa Australia walio katika mkoa wa Uruzgan kabla kuwasili mjini Kabul.