1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Sarkozy ziarani China

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CT39

Rais wa Ufaransa, Nicholas Sarkozy, anafanya ziara rasmi ya siku tatu nchini China. Rais Sarkozy ameitolea mwito China iiruhusu sarafu ya yuan iimarike dhidi ya sarafu ya euro na sarafu nyengine ili kuwepo urari zaidi wa kibiashara.

Rais Nicolas Sarkozy atakutana na rais wa China, Hu Jintao, hii leo. Ziara ya rais Sarkozy, iliyoanza jana, inatarajiwa kutuwama juu ya ushirikiano wa kiuchumi na maswala ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Lakini wakati wa chakula cha jioni pamoja na rais Hu Jintao, hapo jana, rais Sarkozy kwa upole aliishawishi China isiitumie mara kwa mara hukumu ya kifo na kuitaka iulinde uhuru wa waandishi wa habari wanaofanya kazi nchini humo.

Rais Sarkozy pia ameitaka China ijihusishe zaidi katika kutafuta suluhisho la mgogoro wa Myanmar.