1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Sarkozy ziarani Mashariki ya Kati

14 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CpAX

RIYADH

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amewasili nchini Saudi Arabia katika kituo chake cha kwanza cha ziara ya nchi tatu Mashariki ya Kati.

Akiwa mjini Riyadh amekutana na Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia kujadili ongezeko la bei za mafuta.Rais huyo wa Ufaransa pia ameliambia gazeti la kizalendo la Kiarabu Al –Hayat kwamba anapanga kutia saini ushirikiano wa matumizi ya nuklea kwa shughuli za kiraia na Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo anatazamiwa kuwasili hapo kesho.

Ufaransa imetia saini makubaliano kama hayo na Libya na Algeria hivi karibuni.