1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Uhuru aanza kutatua tatizo la ardhi Kenya

Josephat Nyiro Charo4 Septemba 2013

Utoaji wa hati za kumiliki ardhi umeleta matumaini makubwa miongoni mwa wakaazi wa Pwani ya Kenya ambao kwa muda mrefu hawajawahi kuona kitu kama hicho kikitendeka.

https://p.dw.com/p/19bZi
Kenya's Deputy Prime Minister and presidential candidate Uhuru Kenyatta smiles as he casts his vote at the Mutomo primary school in Kiambu, north of Nairobi on March 4, 2013 during the nationwide elections. Kenyans went out to vote for presidential, gubernatorial, senatorial elections on March 4, the first since bloody post-poll violence five years ago in which more than 1,100 people died after contested results. AFP PHOTO/SIMON MAINA (Photo credit should read SIMON MAINA/AFP/Getty Images)
Kenia Wahlen Uhuru KenyattaPicha: Getty Images

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amekamilisha zoezi la utoaji wa hati za kumiliki ardhi zaidi ya 60,000 katika jimbo la Pwani hapo siku ya Jumatatu (02.09.2013). Zoezi hilo lilinuiwa kuanza hatua ya kwanza muhimu katika kulitafutia ufumbuzi tatizo sugu la ardhi nchini Kenya. Hata hivyo hatua ya rais Kenyatta imeibua hisia mbalimbali huku wengine wakiisifu na wengine wakiikosoa. Josephat Charo amezungumza na bwana Odenda Lumumba, wa Muungano wa Kitaifa wa masuala ya Ardhi, Natiaonal Land Alliance, na kwanza kumuuliza anazionaje juhudi za rais. Kuyasikiliza mahojiano haya bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Yusuf Saumu