1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Afghanistan ziarani nchini Ujerumani

18 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHu

Düsseldorf:

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan akianza ziara rasmi nchini Ujerumani,amesifu mchango wa jeshi la Ujerumani Bundeswehr katika vikosi vya kuzlinda amani nchini mwake.Rais Karzai amesema mjini Düsseldorf, kwa namna hiyo,hali ya usalama itaimarika nchini Afghanistan na barani Ulaya pia.Kesho rais huyo wa Afghanistan atakwenda Berlin kwa mazungumzo pamoja na kansela Angela Merkel.