1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Rais wa chama cha Imran Khan wa Pakistan atiwa mbaroni

1 Juni 2023

Rais wa chama cha waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan amekamatwa leo katika mji wa mashariki wa Lahore, hayo yakiwa ni kwa mujibu wa shirika la habari la eneo hilo, Geo News.

https://p.dw.com/p/4S4ii
Pakistan | Chaudhry Pervaiz Elahi, ehemalige Ministerpräsident der Provinz Punjab
Picha: ZUMA Press/Imago

Rais huyo, Pervez Elahi anaungana na orodha ndefu ya viongozi wa chama hicho cha Pakistan Tahreek-e-Insaf, ambao wamekamatwa kaika misako ya wiki za hivi karibuni na kuwekwa kizuizini.

Kukamatwa na Imran Khan mwenyewe kulisababisha maandamano makubwa, yaliyoibua wasiwasi juu ya utengamano wa Pakistan wakati taifa hilo la kusini mwa Asia likipambana na mgogo wa kiuchumi mkubwa zaidi katika kipindi cha miongo mingi.

Waziri wa habari katika jimbo la Punjab Amir Mir, amesema Elahi anakabiliwa na mashitaka ya ubadhirifu, na kwamba amekuwa akitafutwa kwa siku kadhaa zilizopita.