1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran aulaumu Umoja wa Mataifa

Abou Liongo26 Septemba 2007

Rais Mahamoud Ahmednejad wa Iran amevilaumu vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo na Umoja wa Mataifa akisema ni kinyume na sheria.

https://p.dw.com/p/CB0z
Rais Mahmoud Ahmednejad wa Iran
Rais Mahmoud Ahmednejad wa IranPicha: AP

Akihutubia mkutano wa baraza Kuu la Umoja huo mjini New York, Kiongozi huyo wa Iran alisema suala la mzozo wa mpango wa nuklia wa nchi hiyo sasa limefungwa na kwamba hivi sasa liko katika mikono ya shirika la kimataifa la nguvu za atomic.

Mapema Rais Nicolaus Sarkozy alisema mpango wa nuklia wa Iran ni hatari kwa dunia.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel naye kwa upande wake akihutubia mkutano huo alisema kuwa Iran inatakiwa kuishawishi dunia ya kwamba haina nia ya kutengeza bomu la nuklia, vinginevyo itaunga mkono vikwazo zaidi dhidi yake.

Rais Ahmednejad katika hotuba yake hiyo ambapo wajumbe wa Marekani na Israel walitoka nje wakati akiisoma alilaumu kile alichokiita kiburi, udhalimu na uonevu unaofanywa na wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuiwekea nchi hiyo vikwazo.

Kiongozi huyo wa Iran alilitaka Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutilia maanani tofauti iliyopo kati ya mataifa yaliyoendelea kiviwanda duniani na yale yanayoendelea.