1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Jamhuri ya Czeki ahimizwa kuidhinisha Mkataba wa Lisbon

5 Oktoba 2009

Viongozi wa Umoja wa Ulaya walipumua baada ya Mkataba wa Lisbon kuungwa mkono na wapiga kura nchini Ireland mwisho wa juma lililopita.

https://p.dw.com/p/Jxw1
Czech Republic's President Vaclav Klaus attends a demonstration opposing the Lisbon Treaty in Prague, Czech Republic, Saturday, Oct. 3, 2009. Czech President Vaclav Klaus declined to say today how he would proceed in ratification of the European Union's Lisbon Treaty after the document was approved by Irish voters in a referendum. (AP Photo/Petr David Josek)
Rais wa Jamhuri ya Czeki,Vaclav Klaus akihudhuria maandamano ya kupinga Mkataba wa Lisbon mjini Prague.Picha: AP

Lakini mkataba huo wa Umoja wa Ulaya uliofanyiwa marekebisho bado unahitaji kuidhinishwa na Poland na Jamhuri ya Czeki ili uweze kutumika ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2009.

Mkataba wa Umoja wa Ulaya unaojulikana kama Mkataba wa Lisbon uliungwa mkono na asilimia 67 ya wapiga kura nchini Ireland mwisho wa juma lililopita, kinyume kabisa na vile ulivyokataliwa mwaka uliopita. Lakini mkataba huo ulio na azma ya kurahisisha utaratibu wa kupitisha maamuzi katika Umoja wa Ulaya na kubuni nyadhifa za rais na waziri wa mambo ya nje wa umoja huo, unaweza tu kutumika ikiwa utaidhinishwa na wanachama wawili wa mwisho - Poland na Jamhuri ya Czeki.

Rais wa Poland Lech Kaczynski anatazamiwa kutia saini mkabata huo hivi karibuni. Lakini Rais wa Jamhuri ya Czeki Vaclav Klaus, mkosoaji mkubwa wa Umoja wa Ulaya, ameshasema kuwa yeye hatotia saini mpaka Mahakama ya Katiba ya nchi yake itakapoamua iwapo mkataba huo unakikuka katiba ya nchi au la. Na uamuzi wa mahakama huenda ukachukua wiki kadhaa.

David Cameron, Britain's leader of the Conservative Party, delivers his keynote speech on the last day of the Conservative Party conference in Blackpool, England, Wednesday, Oct. 3, 2007. The annual Conservative Party conference runs for four days. (AP Photo/Kirsty Wigglesworth)
David Cameron, kiongozi wa chama cha kihafidhina nchini Uingereza.Picha: AP

Hata hivyo, Rais Klaus si mkosoaji pekee wa Umoja wa Ulaya. Kwani nchini Uingereza, kiongozi wa chama cha upinzani cha Conservative David Cameron amesema waziwazi kuwa chama chake kikishinda uchaguzi mkuu utakaofanywa mwakani, basi kitaitisha kura ya maoni kama hadi hapo, mkataba huo haukuidhinishwa na wanachama wote 27 katika Umoja wa Ulaya. Akifafanua sababu za lawama zake amesema, tatizo ni kwamba mkataba huo unazipokonya nchi madaraka yake na kuyapeleka Umoja wa Ulaya na chama chake, hakiamini kuwa huo ni utaratibu wa maana.

Lakini kwa maoni ya Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown wa chama cha Labour, matokeo ya kura zilizopigwa siku ya Ijumaa nchini Ireland yamefungua njia kwa Umoja wa Ulaya kushughulikia masuala yaliyo muhimu zaidi kwa wananchi wao - kuimarisha uchumi,usalama, kupambana na umasikini duniani na mabadiliko ya hali ya hewa.

Hata Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa amefurahi sana, kwani hatua iliyochukuliwa na Ireland ni hatua muhimu sana kuelekea kutekelezwa kwa Mkataba wa Lisbon. Matokeo ya nchini Ireland yamekaribishwa pia katika nchi za Balkan zilizohofia kuwa kukataliwa kwa mkataba huo kwa mara ya pili kutaondosha uwezekano wa nchi hizo kupokewa kama wanachama katika Umoja wa Ulaya.

Mwandishi: P.Martin/RTRE/AFPE

Mhariri: M.Abdul-Rahman