1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina achukua uongozi

John Juma
17 Novemba 2023

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina anashikilia uongozi wa mapema katika zoezi la kuhesabiwa kwa kura za uchaguzi mkuu uliofanyika jana Alhamisi.

https://p.dw.com/p/4Z3o3
Andry Rajoelina | madagassischer
Rais wa Madagascar Andry RajoelinaPicha: Abd Rabbo Ammar/ABACA/IMAGO

Rajoelina anawania kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo ya kisiwa. Upinzani ulisusia uchaguzi huo ambao wapiga kura wachache ndio walijitokeza.

Kulingana na matokeo ya awali, Rajoelina mwenye umri wa miaka 49, amejikingia zaidi ya asilimia 72.9 ya kura zote ambazo zilikwishahesabiwa na tume inayosimamia uchaguzi nchini humo CENI.

Tume hiyo imesema kura zilizohesabiwa kufikia sasa zimeonyesha ni asilimia 39.5% ya wapiga kura ndio walijitokeza ikilinganishwa na asilimia 55 katika uchaguzi wa mwaka 2018.