1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Misri el-Sissi aahidi kuwalinda wananchi maskini

Oumilkheir Hamidou
30 Septemba 2019

Rais wa Misri Abdel-Fattah el Sissi asema hatua zinafanyika kulinda haki za watu walioathirika kufuatia kuondolewa ruzuku.

https://p.dw.com/p/3QULS
Symbolbild Ägypten Präsident Abdel-Fattah el-Sissi
Picha: picture-alliance/AP Photo/MENA

Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi amesema atawalinda wananchi wake masikini na wenye kipato cha kati wanaokabiliwa na hali ngumu kutokana na hatua za serikali yake za kubana matumizi. Ni mara ya kwanza rais el Sissi ametowa kauli juu ya uchumi kufuatia maandamano yasiyokuwa ya kawaida ya kuipinga serikali, yaliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu ambayo inaaminika kwa sehemu yamechochewa na hali ngumu ya kiuchumi. Maandamano hayo yalisababisha kuchukuliwa hatua kubwa za kiusalama. Kupitia ujumbe wa Twitta ulioandikwa Jumapili usiku el Sissi alisema hatua zinafanyika kulinda haki za watu walioathirika kufuatia kuondolewa ruzuku. Rais El Sissi alianzisha mpango wa mageuzi mwaka 2016 wenye lengo la kuuimarisha uchumi wa nchi hiyo uliopwaya.