1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Rais wa Poland kumtangaza waziri mkuu mpya

Saumu Mwasimba
6 Novemba 2023

Rais wa Poland anatarajiwa kumtangaza waziri mkuu mpya wa nchi hiyo,katika hatua ambayo imesubiriwa kwa wiki kadhaa baada ya chama tawala cha wazalendo kupoteza uungaji mkono katika uchaguzi wa bunge wa Oktoba 15.

https://p.dw.com/p/4YTes
Rais wa Poland Andrzej Duda
Rais wa Poland Andrzej DudaPicha: Beata Zawrzel/NurPhoto/picture alliance

Rais Andrzej Duda mshirika wa chama cha PiS alisema kabla ya uchaguzi kwamba atajaribu kuunda serikali ya chama kimoja kikubwa.

Kufuatia mashauriano na kutafakari kwa kina rais Duda amefanya maamuzi yake kuhusiana na kile kinachoonekana kuwa hatua ya mwanzo ya uteuzi wa serikali yake.

Soma pia:Muungano wa upinzani wafanikiwa wingi wa viti Poland

Kupitia ujumbe ulioandikwa katika mtandao wa X na mkuu wa shughuli za ofisi ya rais huyo,imebainika kwamba rais Duda anatarajiwa kulihutubia taifa  jioni hii moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni cha taifa kutangaza waziri mkuu aliyemteua.

Miongoni mwa wanaotajwa kuwa nafasi kutangazwa kuchukuwa wadhifa huo ,ni waziri mkuu anayeondoka Mateusz Morawiecki, na Donald  Tusk.