1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Rushia Vladimir Putin aitembelea Ujerumani

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD47

Rais wa Rushia, Vladimir Putin, anaanza leo ziara yake ya siku mbili hapa Ujerumani. Katika hatua ya kwanza ya ziara hiyo, rais Putin amepangiwa kukutana kwa mazungumzo na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, katika mji wa Dresden mashariki mwa nchi. Miongoni mwa maswala yatakayozungumziwa ni pamoja na mauwaji ya muandishi wa habari wa Rushia Anna Politkovskaya mjini Moscow mwishoni mwa wiki iliopita pamoja pia na mzozo unaoendelea kati ya Rushia na Georgia.