1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete azungumzia kuhusu ugonjwa wa malaria

Josephat Nyiro Charo27 Julai 2010

Rais Kikwete asema ufanisi mkubwa umepatikana katika vita vya kupambana na ugonjwa hatari wa malaria. Hata hivyo changamoto bado zingaliko katika kuutokomeza ugonjwa huo barani Afrika

https://p.dw.com/p/OW3e
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa TanzaniaPicha: AP Photo

Kwenye mkutano wa marais wanachama wa umoja wa Afya uliomalizika jana mjini Kampala, marais wa nchi za umoja huo walifanya mkutano kujadili hatua ambazo Afrika imepiga kwenye vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria. Marais hao walikutana chini ya mwavuli wa muungano wa viongozi wa Afrika wa kupambana na Malaria, kwa kifupi ALMA.

Mwandishi wetu Leyla Ndinda ametutumia taarifa ifuatayo

Mwandishi: Leyla Nidnda

Mhariri:Josephat Charo