1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ufaransa ziarani China

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CStb

Beijing:

Rais Nicholas Sarkozy wa Ufaransa amewasili Beijing kwa ziara rasmi ya siku tatu katika jamhuri ya umma wa china.Leo usiku rais Sarkozy amepangiwa kukutana na rais Hu Jintao.Mada kuu mazungumzoni ni kuhusu sera za maendeleo barani Afrika,usafi wa mazingira na ushirikiano wa kiuchumi.Rais Nicolas Sarkozy anapanga kuwashi viongozi wa China wakubali kununua ndege chapa ya Airbus pamoja na zana nyenginezo za kiufundi za Ufaransa.Mashirika ya haki za binaadam yanahofia masuala ya haki za binaadam yasije yakasahauliwa wakati wa mazungumzo mkati ya rais Sarkozy na viongozi wa jamhuri ya umma wa China.