1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani ziarani Uganda

4 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1rb

KAMPALA:

Rais Horst Köhler wa Ujerumani amewasili Uganda akiwa katika ziara ya siku sita barani Afrika itakayompeleka Rwanda vile vile.Alipowasili Kampala,alipokewa na rais mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni.Hii ni ziara ya tano kufanywa na Rais wa Ujerumani barani Afrika,tangu kushika madaraka mwaka 2004.