1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WADA: visa vya udanganyifu katika riadha hugunduliwa

14 Agosti 2015

Rais wa Shirika la Kimataifa la Kupambana na Matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni – WADA Craig Reedie ameutetea mchakato unaotumiwa katika riadha akisema kuwa visa vya udanganyifu hugunduliwa.

https://p.dw.com/p/1GFiI
WADA Präsident Craig Reedie
Picha: picture-alliance/dpa/L.Schulze

Akiyajibu madai ya hivi karibuni ya vyombo vya habari, ya kugunduliwa mamia ya matokeo ya vipimo vya damu katika miaka ya karibuni, Reedie amesema kuwa madai hayo hayawezi kuthibitishwa kisayansi na kisheria. "Sidhani kama ina maana kuwa watu wanatumia dawa za kuongeza nguvu. Vipimo vya kwanza vya damu ambavyo vimetolewa wazi ni vipimo huru na hauwezi kuzingatia tuhuma ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kwa kipimo kimoja cha damu, hilo haliwezi kujitosheleza kisayansi na kisheria".

Shirikisho la kimataifa la riadha – IAAF lilisema mapema wiki hii kuwa kesi 32 kuu za matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini zinazowahusisha wanariadha 28 zimefichuliwa baada ya uchunguzi mpya wa vipimo vilivyochukuliwa karibu mwongo mmoja uliopita.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Daniel Gakuba