1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Zanzibar amwachisha kazi Mansoor Yussuf Himid

16 Oktoba 2012

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein amemwachisha kazi Waziri asiyekuwa na wizara maalum Mansoor Yussuf Himid na kumteua Bi Shawana Buheti Hassan kuchukua wadhifa huo.

https://p.dw.com/p/16QfP
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed SheinPicha: DW

Hatua hiyo hata hivyo imekuja wakati ambapo Zanzibar ipo katika harakati za kutaka mabadiliko ya mfumo wa Muungano na Bwana Mansoor amekuwa mstari wa mbele katika mchakato huo wa kutetea mageuzi. Hatua hiyo ya rais imezusha hisia mbali mbali miongoni mwa wananchi wa visiwa hivyo. Bruce Amani amezungumza na mchambuzi wa siasa Prof. Abdul Shariff, na kwanza alimuuliza je hatua hiyo iliyochukuliwa na rais inatoa sura gani.

Mwandishi: Bruce Amani

Mhariri: Saumu Yusuf