1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais William Ruto atimiza mwaka mmoja madarakani

Saumu Mwasimba
13 Septemba 2023

Serikali ya Kenya inayoongozwa na rais William Ruto na chama chake cha Kenya Kwanza, imetimiza mwaka mmoja madarakani, tangu ilipoingia madarakani baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata.

https://p.dw.com/p/4WHZX
Der keniansiche Präsident William Ruto in Südafrika
Picha: Ihsaan Haffejee/AA/picture alliance

Hadi sasa, wakenya wanalalamikia ughali wa maisha kutokana na ongezeko la bei za bidhaa na mafuta ya petroli. 

Serikali hiyo ya Kenya inashikilia kwamba imefanikiwa kuurekebisha  uchumi kwa misingi ya kulipunguza deni baada ya kuongeza mapato ya kodi kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2023.

Rais Ruto awaomba wapinzani Kenya kutoa nafasi kwa mazungumzo

Mapema mwezi wa Agosti mwaka huu, Rais William Ruto alishikilia kuwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki haiwezi kuongozwa kwa kutegemea  mikopo na kwahivyo hatua za kuongeza kodi ili kuimarisha pato la taifa ni ya lazima.Upinzani unaoongozwa na Raila Odinga bado hauna imani na serikali hiyo ya Kenya.