1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLA : Rice akutana na Rais Abbas

5 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79n

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice amekutana na Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina katika mji wa Ukingo wa Magharibi wa Ramallah.

Mkutano huo unakuja siku moja baada ya Rice kukutana na viongozi wa Israel mjini Jerusalem kujadili juhudi za pande hizo mbili kukubaliana juu ya mada kuu za mkutano wa amani wa Mashariki ya Kati ulipangwa kufanyika nchini Marekani.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Tzipi Livni amemuambia Rice kwamba usalama wa Israel inabidi uzingatiwe kwanza kabla ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote yale.

Rice amesema kwamba mkutano huo wa amani ya Mashariki ya Kati unaodhaminiwa na Marekani utatowa fursa halisi ya kuendeleza mbele lengo la kuanzisha taifa huru la Wapalestina lenye amani.