1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Abbas na Haniyeh wanajaribu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCs3

Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Wapalestina na waziri mkuu Ismail Haniyeh wa chama tawala cha Hamas wameshindwa kukubaliana kuhusu serikali ya umoja wa taifa iliyopendekezwa kuundwa.Afisa mmoja wa Kipalestina amesema,hata hivyo mkutano huo unaofanywa mahala pa siri katika mji wa Gaza utaendelea.Tangu siku chache za nyuma,Abbas anaekiongoza chama cha Fatah chenye siasa za wastani na maafisa wa Hamas,wamekuwa wakisema kuwa wanakaribia kuunda baraza la mawaziri la serikali mpya,baada ya utaratibu huo kukwama kwa miezi kadhaa.Wakati huo huo,maafisa wa Hamas wa ngazi ya juu wamesema hawatoitambua Israel, hawatoheshimu mikataba iliyotiwa saini pamoja na taifa la Kiyahudi na wala hawatotangaza kuacha matumizi ya nguvu.Nchi za magharibi zimesema hazitoanza kutoa msaada wa moja kwa moja kwa serikali ya Wapalestina,mpaka masharti hayo yatakapotimizwa.