1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Abbas na Olmert wapo tayari kuendeleza mchakato wa amani

3 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBce

Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas amesema,yupo tayari kujadiliana na Israel “masuala ya kimsingi“ yanayohusika na kuundwa kwa taifa la Palestina.Alisema hayo baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice mjini Ramallah.

Hapo kabla,Rice alimuarifu Abbas,kuwa Israel ipo tayari kujadili „kanuni za kimsingi“ ili kuendeleza mchakato wa amani uliokwama.

Condeleezza Rice ameshamaliza ziara yake ya siku nne katika Mashariki ya Kati.Ziara hiyo ilikuwa na azma ya kufanya maandalizi ya mkutano wa amani kuhusu Mashariki ya Kati.Mkutano huo wa kimataifa umependekezwa na Rais wa Marekani,George W.Bush kufanywa baadae mwaka huu.