1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : Kaburi kubwa la Arafat lazinduliwa

10 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBKB

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina leo amezinduwa kaburi kubwa lililogharimu euro milioni moja na laki mbili kwa ajili ya marehemu Yasser Arafat miaka mitatu baada ya kufariki kwa kiongozi huyo wa Wapalestina.

Akizungumza mjini Ramallah katika Ukingo wa Magharibi Abbas amesema iko siku watamzika upya Arafat katika mji wa Jerusalem ambako ndiko alikozaliwa na mji aliokuwa akiupemda na ambao wananchi wa Palestina wanataka uwe mji mkuu wa taifa lao.

Wapalestina na wanadiplonmasia wa kigeni wamehudhuria kumbukumbu hiyo ya miaka mitatu ya kifo cha Arafat ambaye anasifiwa kwa kuyafikisha mapambano ya Wapelstina katika jukwaa la kimataifa.