1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Majeshi ya Israil yashambulia Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusababisha mauaji.

5 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdC

Kiasi Wapalestina wanne wameuawa na wengine 20 wamejeruhiwa baada ya wanajeshi wa Israil kuuvamia mji wa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wanajeshi hao wamesema waliuvamia mji huo ili kuwakamata wanamgambo wanne wa kipalestina.

Uvamizi huo ulitokea huku mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Israil, Ehud Olmert, na Rais wa Misri, Hossni Mubarak, ukiendelea katika mji wa Sharm el-Sheikh kando mwa bahari ya Sham.

Mara baada ya mkutano huo, Mubarak alielezea kufadhaishwa na uvamizi huo.

Waziri Mkuu Ehud Olmert alisema alisikitishwa na maafa yaliyotokea, lakini akasisitiza kwamba serikali yake ina jukumu la kuwalinda raia wake.

Mkutano kati ya viongozi hao wawili ulinuiwa kuchunguza jinsi ya kuanza upya mashauriano ya amani kati ya Israil na Wapalestina.