1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : PLO yataka serikali ya Hamas ijiuzulu

2 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnP

Kamati Kuu ya chama cha Ukombozi wa Palestina PLO imetowa wito kwa serikali ya Hamas kujiuzulu ikiwa ni sharti la kuanza tena mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina na kundi hilo la wanamgambo wa Kiislam.

Kamati hiyo Kuu ya PLO ilikutana hapo jana baada ya Rais wa msimamo wa wastani Mahmoud Abbas kutangaza kwamba mazungumzo yake na Hamas juu ya kuunda serikali ya msimamo wa wastani itakayokubalika na mataifa ya magharibi yameshindwa.

Katika taarifa uongozi wa PLO umesema kwamba serikali inayoongozwa na Hamas lazima ijiuzulu kutowa nafasi ya kuchaguliwa kwa serikali mpya.

Waziri Mkuu wa Palestina Ismael Haniyeh huko nyuma alimwambia Rais Abbas kwamba atajiuzulu pale tu yatakapokuwa yamefikiwa makubaliano ya kuundwa kwa serikali mpya.