1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Rais wa Wapalestina huenda akaitisha mapema uchaguzi

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkt

Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas ataitisha mapema chaguzi za rais na bunge ikiwa atashindwa kuunda serikali mpya,kuchukua nafasi ya serikali ya Hamas inayosusiwa na nchi za magharibi.Yasser Abed Rabbo alie mwanachama wa baraza la maamuzi la chama cha PLO,alitamka hayo alipozungumza na waandishi wa habari,baada ya baraza hilo kushauriana hatua gani ichukuliwe na rais Abbas aliesema kuwa mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja na Hamas yamekwama.