1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Serikali ya dharura ya Wapalestina imeapishwa Ukingo wa Magharibi

17 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqy

Serikali mpya ya dharura ya Wapalestina imeapishwa hii leo mjini Ramallah,kwenye Ukingo wa Magharibi.Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah,amelitangaza baraza jipya la mawaziri baada ya kuivunja serikali ya umoja wa kitaifa kati ya Hamas na Fatah.Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya wanamgambo wa Hamas kuudhibiti Ukanda wa Gaza,kufuatia mapigano makali.kwa upande mwingine,Israel imekaribisha uteuzi wa baraza hilo jipya la mawaziri.Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert amesema,serikali isiyokuwa na mawaziri kutoka chama cha Hamas, inaashiria nafasi mpya ya kupata amani.