1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH:Rice azitaka Israel na Palestina kutayarisha ajenda ya pamoja

26 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condeleza Rice amependekeza kuwepo na mazungumzo sambamba ya kidiplomasia kati ya viongozi wa Israel na Palestina, ili kubuni ajenda ya pamoja itakayofufua mazungumzo ya mpango wa amani wa Mashariki ya Kati.

Condeleza Rice alisema hayo hapo jana mjini Ramallah baada ya mazungumzo yake na Rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahamoud Abbas.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon pia alikutana na Abbas na akataka serikali mpya ya Palestina ikubaliane na matakwa ya kimataifa kuhusiana na Israel.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Marekani alikutana pia na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmet, kabla hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kukutana na Waziri Mkuu huyo wa Israel.

Ziara hizo za Condeleza Rice na Ban Ki-Moon zinafanyika kabla ya mkutano wa wakuu wa nchi za kiarabu hapo siku ya Jumatano mjini Riyadh Saudi Arabia.