1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH:SteinMeir atangaza mpango wa EU juu ya kuimarisha usalama mashariki ya kati

1 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7As

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Stein Meir ambaye yuko ziarani katika mashariki ya kati amekutana na waziri mkuu wa Palestina Salam Fayyad ukingo wa Magharibi.Steinmeir ameutumia mkutano huo kutangaza mpango wa Umoja wa Ulaya wa kuimarisha usalama katika eneo hilo la mashariki ya kati.Amesema mpango huo utajumuisha utaratibu wa kuimarisha biashara za viwango mbali mbali za wapalestina, vyuo vikuu katika ukingo wa magharibi,pamoja na taasisi mbali mbali za serikali.Ziara ya waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani kwenye neo la mashariki ya kati ni juhudi mojawapo ya maandalizi kwa ajili ya mkutano wa kilele unaodhaminiwa na Marekani juu ya amani ya mashariki ya kati utakaofanyika baadae mwezi huu.