1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah.wakati Wapalestina wataka kusitishwa kwa mapigano, Israel yaendelea kufanya hujuma.

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpp

Makundi ya wanamgambo wa Palestina kimsingi yamekubaliana kusitisha mapigano na Israel.

Tangazo hilo limekuja baada ya mkutano na waziri mkuu Ismail Haniya huko Gaza.

Kiongozi wa kundi la Islamic Jihad Khader Habib aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wawakilishi kadhaa wa kitaifa na makundi ya waislamu walikutana na Haniya na kukubali kusitisha mashambulizi, kwa sharti kwamba Israel nayo itaridhia.

Hata hivyo Israel imelikataa shauri hilo, na kusema kuwa itasimamisha operesheni zake za kijeshi baada ya wanamgambo kuweka chini silaha zao.

Wakati huo huo mwanamgambo mmoja kutoka katika tawi la kijeshi la chama cha Hamas ameuwawa hii leo kufuatia mashambulizi ya Israel huko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza wakati vikosi hivyo vikifanya operesheni dhidi ya mashambulizi ya marokrti.

Chanzo cha habari kutoka Palestina kimesema, Ayman Juda mwenye umri wa miaka 22 ameuwawa kwa kupigwa risasi na Israel huko Beit Lahiya.

Kifo cha Juda kinafanya idadi ya watu waliouwawa kutokana na mashambulizi ya Israel tangu mwaka 2000 kufikia 5,592 wengi wao wakiwa ni wa-Palestina.

Aidha jeshi la Israel siku ya Jumatatu lilifanya operesheni kubwa ya kijeshi ya ardhini huko kaskazini mwa ukingo wa Gaza.

Katika operesheni hiyo ilipelekea kuuwawa kwa watu 12 na zaidi ya 20 kujeruhiwa.