1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMMALLAH:Steinmeir ziarani mashariki ya kati

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4J

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amezitaka nchi za mashariki ya kati kukikumbatia kile alichokitaja kuwa ni nafasi nadra ya kutafuta amani.

Amesema uamuzi wa nchi za umoja wa kiarabu wa kufufua mpango wa amani umeunda nafasi ambazo hazikuwepo katika siku za nyuma.

Waziri Steinmeir ameyasema hayo kufuatia mkutano na mwenzake wa Palestina Ziad Abu Amr pamoja na waziri wa fedha Sallam Fayyad huko ukingo wa magharibi.

Waziri wa mambo ya nje wa Palestina Ziad Abu Amr amemuomba waziri Steinmeir kuishawishi Israel iwachilie mamilioni ya dolla za wapalestina ambazo imezizuia.

Waziri Steinmer amepangiwa kukutana na viongozi wa Israel jumatatu.