1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rangon . Suu Kyi atembelewa na afisa wa umoja wa mataifa.

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtj

Afisa wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa amekutana na kiongozi anayependelea demokrasi nchini Burma ambaye amezuiliwa nyumbani kwake Aung San Suu Kyi mjini Rangoon.

Ibrahim Gambari amesema mshindi huyo wa nishani ya amani ya Nobel mwenye umri wa miaka 61 alimweleza kuwa yuko katika hali nzuri kiafya lakini alikuwa anahitaji kutembelewa mara kwa mara na daktari wake.

Ofisi ya umoja wa mataifa mjini Yangon imesema kuwa Gambari pia amekutana na kiongozi wa uongozi wa kijeshi wa Burma , jenerali mkuu Than Shwe.

Lakini ofisi hiyo haikutoa maelezo zaidi juu ya mazungumzo yao, ikisema kuwa mazungumzo hayo yametuwama katika masuala kadha ya kisiasa na kiutu.

Chama cha National League for Democracy cha Suu Kyi , kilishinda uchaguzi wa mwaka 1990 nchini Burma , lakini jeshi lilitupilia mbali matokeo hayo.

Amekuwa chini ya aina fulani ya ulinzi kwa zaidi ya miaka 10 kati ya 17 iliyopita.