1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rangoon. Watawa waandamana tena.

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Aw

Kiasi cha watawa 200 nchini Burma wamefanya maandamano katikati ya nchi hiyo , mara ya kwanza kufanya hivyo tangu utawala wa kijeshi nchini humo kuzima maandamano yaliyokuwa yakiongozwa na watawa hao.

Watawa walifanya maandamano yao katika mji wa Pakokku. Wakati wa maandamano yaliyofanyika katika mwezi wa Septemba maandamano ambayo yalianzia katika mji wa Pakokku, viongozi wa kijeshi wa Burma walisema kuwa watu kumi waliuwawa. Serikali za mataifa ya magharibi zilidai kuwa idadi ya watu waliouwawa ilikuwa juu zaidi. Mwakilishi maalum wa umoja wa mataifa Ibrahim Gambari anatarajiwa kurejea nchini Burma mwishoni mwa juma hili kuwahimiza majenerali wa Burma kunzisha mazungumzo na kiongozi wa upinzani aliye kizuizini Aung San Suu Kyi.