1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RANGOON:Watawa na wananchi wakaidi amri ya kukomesha maandamano

26 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMU

Vikosi vya usalama nchini Myanmar vimetumia gesi za kutoa machozi pamoja na kufyatua risasi hewani kuwatawanya watawa wa kibudha waliokaidi amri ya kukomesha maandamano hii leo.

Watawa hao walizuia kuingia kwenye madhabahu ya mjini Rangoon.

Hatua hii imechukuliwa na vikosi vya usalama baada ya serikali kutangaza amri ya kutotembea ovyo na mikutano hapo jana usiku.Taarifa zinasema baadhi ya wanaharakati hao wa kutetea demokrasia walikamatwa.Katika kipindi cha siku nane zilizopita watu zaidi ya laki moja wamekuwa wakiandamana katika miji mikubwa nchini Myanmar zamani ikiitwa Burma.Kufuatia hali hii rais Bush hapo jana alitumia hotuba yake katika mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa kutangaza vikwazo zaidi vya usafiri dhidi ya viongozi wa nchi hiyo na wafadhili wao wa kiuchumi.