1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rashia-Georgia

Hamidou, Oumilkher23 Agosti 2008

Maandamano karibu na Gori dhidi ya vikosi vya Urusi nchini Georgia

https://p.dw.com/p/F3c9

GORI:


Vikosi vya Georgia vinaidhibiti njia muhimu inayounganisha sehemu ya mashariki na ile ya magharibi ya nchi hiyo,baada ya vikosi vya Urusi kuihama sehemu hiyo.Kiongozi wa pili wa vikosi vya wanajeshi vya Urusi,jenerali Anatoli NOGOVITSINE amehakikisha hii leo "nyendo zote za wanajeshi wa Urusi zinaambatana na ahadi za Moscow kwa mkataba wa vifungu sita wa kuweka chini silaha."Akizungumza na waandishi habari naibu amiri jeshi huyo wa Urusi amesema hata hivyo vikosi vya nchi yake vitaendelea kupiga doria katika bandari ya mji wa Poti nchini Georgia.Akiulizwa kuhusu wanajeshi wa Urusi walioko karibu na bahari nyeusi,jenerali Anatoli Nogovitsine amejibu akisema jambo hilo ni miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Urusi na Ufaransa.Viongozi wa serikali ya Georgia wamezisuta hoja hizo.Wizara ya mambo ya ndani imesema mjini Tblissi,vikosi vya Urusi bado vinakutikana katika maeneo ya karibu na Poti.Na ripota wa shirika la habari la Reuters amezungumzia juu ya kuwekwa vizuwizi vya Urusi katika kijiji cha Karaleti,umbali wa kilomita sita karibu na mji wa Gori.Maandamano yamefanyika leo dhidi ya kuwepo vikosi vya Urusi karibu na Gori.Marekani,Ufaransa zinaikosoa Urusi kwa kutoheshimu makubaliano ya kuweka chini silaha.Na Uengereza pia imeelezea wasi wasi kuhusu suala hilo.