1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raundi ya pili ya mechi za makundi kuanza AFCON

18 Januari 2024

Mechi za makundi za kombe la mataifa barani Afrika AFCON nchini Ivory Coast, zinaingia raundi ya pili leo huku mechi ya kwanza kabisa ikiwapatanisha Guinea ya Ikweta na Guinea Bissau katika uwanja wa Alassana Ouattara

https://p.dw.com/p/4bPhD
AFCON |  Uwanja wa Alassane Ouattara Ebimpé Olympic
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inaendelea Ivory CoastPicha: Braima Darame/DW

Baadae wenyeji Ivory Coast wapambane na Nigeria katika mojawapo ya mechi zinazosubiriwa na wengi.

Kisha timu iliyo na rekodi ya ushindi wa kombe hilo Misri ipambane na ghana katika mchuano wa mwisho siku ya leo. (18.01.2024)

Moroko yaichabanga Tanzania 3-0 AFCON

Hapo jana wawkilishi wa Afrika Mashariki tanzania hawakuwa na jawabu mbele ya Morocco baada ya kunyamazishwa 3-0 halafu Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ikakosa kutumia vyema nafasi zake katika mechi yake na zambia iliyoishia sare ya goli moja.