1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Madrid yaitupa nje Bayern Munich

Sekione Kitojo
19 Aprili 2017

Real Madrid imeifunga Bayern Munich 4-2 katika robo fainali za kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nayo Borussia Dortmund inajaribu kubadili matokeo ya mchezo wa kwanza ambapo ilipigwa 3-2 na Monaco.

https://p.dw.com/p/2bUrc
Champions League Real Madrid vs FC Bayern Munic
Picha: picture alliance/dpa/AP Photo/O. D. Olza

Mchezo  huo uliopangwa  kuchezwa  siku  ya Jumanne uliahirishwa  baada  ya  kutokea  shambulio  la  mabomu dhidi  ya  basi  lililowachukua  wachezaji  wa  Dortmund na hivyo mechi kufanyika  siku iliyofuata  ya  Jumatano.

Basi la Borussia Dortmund lililoshambuliwa
Basi la Borussia Dortmund lililoshambuliwaPicha: Getty Images/M. Hitji

Mchezo  mwingine  ni  kati  ya  FC Barcelona  ikipambana  na Juventus Turin  ya  Italia  ambapo timu  hiyo  ya  jimbo  la  Catalan ina kibarua  kigumu kuweza  kubadilisha  matokeo ya  mchezo  wa  kwanza ya  mabao 3-0. Barcelona  iliweza  kubadilisha  matokeo  ya  kushindwa  kwa  mabao 4-0 dhidi  ya  Paris Saint Germain katika  awamu ya timu  16 katika  Champions League msimu  huu  na  kushinda  kwa  maboa 6-3.

Real Madrid ya  Uhispania ilifanikiwa kuiondoa  Bayern Munich ya  Ujerumani  katika  michuano  ya  kuwania  kombe  la  Ligi  ya  Mabingwa  barani Ulaya, Champions League,  kwa  ushindi  wa  mabao 4-2 ambapo mshambuliaji  nyota  wa  timu  hiyo  Cristiano  Ronaldo  alifunga  mabao matatu. 

Cristiano Ronaldo amefunga goli lake la 100 katika michuano ya Champions League
Cristiano Ronaldo amefunga goli lake la 100 katika michuano ya Champions League Picha: picture alliance/dpa/AA/B. Akbulut

Ronaldo  anakuwa  mchezaji  wa  kwanza  kufunga  mabao 100  katika  Champions League, na  ni  mchezaji  wa  kwanza  kufunga  mabao  matatu  katika  michezo  ya  robo fainali mbili katika  kinyang'anyiro  hicho, baada  ya  kufanya  hivyo  msimu  uliopita. 

Klabu  nyingine  ya Uhispania,  Atletico Madrid, ilifanikiwa  pia  kuingia  katika  nusu  fainali  ya  kombe  hilo  baada  ya  kutoka  sare  ya  bao 1-1  na  mabingwa  wa  England Leicester  City na  kupita  kwa  jumla  ya  mabao 2-1  katika  michezo  miwili  ya  robo  fainali.