1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RI-KWAGBA: Hakuna maafikiano kati ya Egeland na Kony

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtI

Mkuu wa mipango ya kiutu ya Umoja wa Mataifa,Jan Egeland amekuwa na mkutano mfupi pamoja na Joseph Kony alie kiongozi wa kundi la waasi la Uganda la LRA.Mkutano huo umefanywa Ri-Kwagba karibu na mpaka wa Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Egeland alitaka kumshawishi kiongozi wa kundi la LRA awaachilie wanawake na watoto wanaodhaniwa kuwa wafungwa wa kundi hilo,lakini Kony amekanusha tuhuma hizo na hakuna makubaliano yaliopatikana.Joseph Kony anashutumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu.Kwa mujibu wa msemaji wa Kony,waranti ya kutakaa kumkamata ni kizingiti kikubwa katika juhudi za kutafuta amani.Maelfu ya watu wameuawa na kama milioni mbili wengine wamepoteza makazi yao kaskazini mwa Uganda katika vita katili vya miaka 20 kati ya chama cha waasi cha LRA na serikali ya Uganda.