1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ribery na Benzema wakabiliwa na kesi ya ngono

18 Juni 2013

Wachezaji wawili wa kandanda wa timu ya taifa ya Ufaransa Franck Ribery na Karim Benzema wameshtakiwa mahakamani hii leo mjini Paris kwa kutoa malipo ili kushiriki ngono na kahaba mwenye umri mdogo

https://p.dw.com/p/18sQi
Frankreichs Franck Ribery (r), Karim Benzema (l) und Samir Nasri (hinten l) jubeln am Donnerstag (31.05.2012) in Reims in Frankreich beim Länderspiel Frankreich gegen Serbien. Foto: Lejeune
Fußball Ländspiel Frankreich - SerbienPicha: picture-alliance/dpa

Mshambuliaji wa Bayern Munich Ribery na mwenzake wa Real Madrid Karim Benzema wanakabiliwa na adhabu ya hadi miaka mitatu gerezani na faini ya juu ya kiasi cha euro 45,000 kama watapatikana na hatia ya uhalifu huo.

Ribery na Benzema wanakanusha

Wachezaji hao wote wawili wanakanusha mashtaka, na msichana aliyehusika, Zahia Dehar, ametoa ushahidi kuwa wanasoka hao wawili hawakujua kuwa alikuwa na umri wa chini ya miaka 18 wakati walipofanya naye kitendo cha ngono mwaka wa 2008 na 2009.

Zahia Dehar ambaye aliondoa kesi hiyo mahakamani
Zahia Dehar ambaye aliondoa kesi hiyo mahakamaniPicha: Getty Images

Ijapokuwa umri unaoruhusiwa kisheria nchini Ufaransa wa mtu kuwa na ufahamu ni miaka 15, kumlipa yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18, ili kushiriki naye ngono ni uhalifu. Dehar kwa sasa na umri wa miaka 21. Ribery mwenye umri wa miaka 30, alikiri kufanya mapenzi na Dehar, lakini anasisitiza kuwa hakujua kuwa alikuwa na umri mdogo. Benzema naye anakanusha kabisa kufanya kitendo hicho.

Ribery na Benzema hawakustahili kufika mahakamani, huku wakili wa Ribery akisema kuwa kesi hiyo haikuwa na “mwathriwa”, ikizingatiwa kuwa Dehar, aliondoa mahakamani malalamishi yake na “bila mashitaka yoyote”.

Waendesha mashtaka wa serikali waliitaka mahakama hiyo ya Paris itupilie mbali kesi hiyo, wakihoji kuwa wanasoka hao wawili hawakujua kuhusu umri wa Zahia wakati wa uchunguzi wa mwanzo. Jaji hata hivyo aliamua kuwacha kesi hiyo wazi, akisema walistahili kuwa na uwezo wa kutambua kuwa msichana huyo alikuwa na umri mdogo. Kesi hiyo inastahili kudumu kwa takriban wiki moja, na hukumu yoyote huenda ikachukua muda mrefu.

Mwandishi: Bruce Amani/DW

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman