1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rice awasili irak kwa ziara isiyotangazwa

20 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dl8E

Baghdad:

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice amewasili Irak kwa ziara isiyotangazwa. Kabla ya kuwasili nchini humo, Waziri Rice aliyataka mataifa ya kiarabu kufungua uhusiano wa kibalozi na kuipa nafuu ya madeni serikali ya Iraq, kama tunzo kwa juhudi zake za kuboresha hali ya usalama na kuleta upatanishi wa kisiasa nchini humo. Bibi Rice yuko mashariki ya kati kuhudhuria mikutano katika mataifa ya Ghuba, ikiwa ni pamoja na mkutano mmoja nchini Kuwait siku ya Jumanne.

Mwezi uliopita waziri mkuu wa Irak Nuri al-Maliki alianzisha harakati za kijeshi kupambana na wanamgambo wa kishia katika mji wa kusini wa Basra, hali iliozusha mapigano makali na jeshi la wanamgambo hao la Mehdi mjini Basra , miji mengine ya kusini na pia katika mji mkuu Baghdad.