1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Riga. Muungano unaounda serikali waelekea kushinda uchaguzi.

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD56

Wapigakura katika taifa la Latvia katika eneo la Baltic wamepiga kura kuchagua bunge jipya. Ikiwa kiasi cha asilimia 89 za kura zikiwa zimekwisha hesabiwa , matokeo yanaonyesha kuwa muungano wa mrengo wa kati kulia unaoongoza serikali unaelekea kushinda.

Muungano wa vyama vitatu unaoongozwa na waziri mkuu kutoka chama cha Peoples Party aigars Kalvitis umepata asilimia 45 ya kura , na kuiwezesha kupata uwezo wa kumchagua rais na kubaki madarakani.

Kiasi cha Walatvia milioni 1.4 walikuwa na haki ya kupiga kura.