1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIO DE JANEIRO: Marubani wa Marekani kushtakiwa kwa kuua bila kukusudia

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD68

Polisi nchini Brazil inasema marubani wawili wa Marekani huenda wakabiliwe na mashtaka ya kuua bila kukusudia kuhusiana na ajali ya kugongana kwa ndege iliyosababisha ndege ya abiria kuanguka na kuua watu 155 katika eneo la Amazon.

Wanaume hao wawili walikuwa marubani wa ndege moja ya kibiashara iliyogongana na ndege ya shirika la GOL aina ya Boeing 737 – 800 Ijumaa wiki iliyopita.

Ndege hiyo ilifaulu kutua katika kambi ya jeshi abiria wote wakiwa salama.

Imeripotiwa marubani hao watatakiwa kujibu kwa nini waliiendesha ndege hiyo juu mno kupita umbali waliotakiwa.