1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rio de Janeiro. Papa amaliza ziara.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC29

Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Pope Benedict wa 16 amekamilisha ziara yake ya kihistoria nchini Brazil kwa kufungua mkutano wa maaskofu wa eneo la Latin Amrika na Caribian.

Katika ziara yake , Pope amewataka wakaazi wa eneo la Latin Amerika kuendelea kuwa waumini imara wa kile alichokisema kuwa ni msingi wa maadili ya Kikristo.

Pia amezungumzia dhidi ya utoaji mimba.

Zaidi ya watu milioni moja walihudhuria misa ya wazi mjini Sao Paulo siku ya Ijumaa wakati Benedict alipombariki mtakatifu wa kwanza nchini Brazil , mtawa wa Franciscana Antonio de Saint’Ana Galvao.