1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya 2008 ya maripota bila mipaka

30 Desemba 2008

Ripoti ya 2008 inataja waandishi habari 673 waliuliwa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/GPMO

Katika ripoti yake ya mwaka huu unaomalizika 2008 juu ya "UHURU WA WAANDISHI HABARI ULIMWENGUNI" iliotoka leo ,shirika la maripota wasio na mipaka "REPORTERS WITHOUT BORDERS" limetaja kwamba waandishi habari 60 waliuwawa mwaka huu na wengine 673 walikamatwa wakati wakifanya kazi zao.Ripoti inasema pia kuwa waandishi habari 929 walihujumiwa au kutishwa wakati vyombo 353 vya habari zilichuja taarifa zake.

Ripoti ya shirika la "REPORTERS WITHOUT BORDERS"-shirika la maripota wasio na mipaka,imehesabu tu visa ambavyo kumekuwa na mafungamano wazi kati ya kukiukwa kwa uhuru wa waandishi hao na kazi za muandishi. Idadi hizo zilizotajwa zinazungumzia visa tu ambavyo shirika hilo limejulishwa.Haviingizi visa na mikasa ambayo waandshi habari waliokumbwa na visa kama hivyo, hawakuviripoti.Mara nyingi hunyamaa kimya kutokana na sababu za usalama wao.

Kwa lugha nyengine, hii ni njia ile ile ya kukusanya habari na tarakimu kama iliotumiwa miaka ya nyuma kuweka hesabu ya visa na mikasa iliowakuta waandishi habari .

Ukilinganisha na mwaka 2007 ambapo waandishi habari 86 waliuwawa,mwaka huu ni 60.Na wakati mwaka jana waandishi habari 887 walikamatwa mwaka huu idadi ilipungua kidogo ni 673.

Barani Afrika, idadi ya waandishi habari waliokamatwa alao kwa masaa 48, ni kubwa mno .Kwani, huko imegeuka desturi kuwatia waandishi habari nguvuni na magereza ya polisi.Mara nyingi wanapowaudhi viongozi kwa maswali yao au wakiripoti juu ya mada ambazo kwa serikali ni nyeti.

Nchini Iraq, waandishi habari 31 walitiwa mbaroni mwaka huu.Wanajeshi wa kimarekani wakiweka usalama, mara nyingi hupelekea waandishi habari kutiwa kizuizini na sio tu wale wa nchini hata wale wanaotumikia vyombo vya nje vya habari.

Nchini China, jumla ya waandishi habari 38 walikamatwa mwaka huu na kesi nyingi za kuwekwa kizuizini zilihusika na michezo ya Olimpik iliopita.

Nchini Burma,waandishi habari 17 walikamatwa na hasa wale wenye sauti kali walitiwa korokoroni na utawala wa kijeshi.

Ukandamizaji wa waandishi habari na uchujaji habari, umehamia pia katika mtandao wa Internet:kupungua idadi ya waandishi habari waliouliwa au waliotuiwa nguvuni mwaka huu katika vyombo vya habari vya kawaida, hakuna maana kwamba uhuru wa habari umetengenea.Vyombo vya habari kama magazeti,radio na Tv vikijitamnua upande wa mtandao na kuwa mtindo wa kisasa kote duniani,ukaguzi na uchujaji habari unazidi pia upande huo.

Kukandamiza habari zisizopendeza hata katika nchi za kidemokrasia za magharibi, kunazidi.Vita vya kupambana na ugaidi na sheria zilizotungwa baada ya shambulio la Septemba 11 nchini Marekani,kumefanya fani ya taftishi-habari-investigative journalism kuwa ngumu.Waandishi habari wa kigeni hukabiliwa na misukosuko zaidi ikiwa watoka zile nchi ni sehemu au zinafungamana na ushirika unaoongozwa na Marekani kupiga vita ugaidi ulimwenguni.kwa ufupi, hakuna sababu ya matumaini kuwa baada ya dhiki si dhiki, bali faraji kwa waandishi habari ulimwenguni:

Mtindo wa kuwaua waandishi habari unaendelea ingawa idadi yao imepungua kidogo mwaka huu kwa kima cha 22% ukilinganisha na mwaka jana .Vifo vya waandishi habari hutokea sana katika maeneo yenye mizozo mfano wa Iraq,Pakistan,Philipines na Mexico....