1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya Marekani kuhusu mpango wa kinuklea ni hatari-asema waziri mmoja wa israel

Oummilkheir16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcHE

Tel Aviv:

Waziri wa usalama wa ndani wa Israel,Avi Dichter ameikosoa vikali ripoti ya hivi karibuni ya idara za upelelezi za Marekani kuhusu mradi wa kinuklea wa Iran.Hoja kwamba Iran imesitisha mpango wa kutengeneza silaha za kinuklea hazina msingi na zinaweza kusababisha vita-amesema waziri huyo wa usalama wa ndani wa Israel mjini Tel Aviv.Bwana Avi Dichter amesema kitisho cha silaha za kinuklea za Iran kipo na ni jukumu la Israel kuendelea kuitanabahisha Marekani amesisitiza.Israel inaamini Iran itakua imeshajitengenezea bomu la kinuklea hadi ifikapo mwaka 2010.