1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya OECD na Ujerumani

21 Oktoba 2008

Umasikini unaongezeka nchini ujerumani hasa kwa watoto.Mwanya kati ya wanaopata pato la juu na la chini ni mkubwa.

https://p.dw.com/p/FeGF

Kutokana na msukosuko wa fedha ulimwenguni, hata mishahara minono ya mameneja wa mabanki nchini Ujerumani, imeingia sasa katika kashfa.Mameneja wanapata mishahara i ya mamilioni wakati wafanyikazi wa kawaida wanaondokea na Euro mia kadhaa tu kwa mwezi.

Uchunguzi mpya uliochapishwa hivi punde na Shirika la Maendeleo ya Kiuchumi na Ushirikiano (OECD )umebainisha kuwa, mwanya kati ya wale wanaovuna mishahara mikubwa na wale wanaopata mishahara midogo nchini Ujerumani , umepanuka mnamo miaka michache iliopita.Ukosefu huu wa usawa umeongoza katika hali ya umasikini kwa sehemu ya jamii.

Kwa muujibu wa ripoti iliochapishwa leo mjini Paris,Ufaransa,umasikini na kutokuwapo mapato sawa kumeongezeka nchini Ujerumani mnamo miaka michache iliopita kuliko katika nchi nyengine za OECD. Kuanzia mwaka 2000 hadi 2005, kiasi cha 10.5 hadi 11% ya wakaazi wa Ujerumani, wanaishi kwa pato lililochini ya kipimo cha masikini.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990 kiwango cha umasikini nchini Ujerumani, kilikuwa kiasi robo kasoro ya kima cha sasa kilichoelezwa na shirika la OECD.Hivi sasa kimepindukia kima cha wastani cha nchi 30 zanachama wa shirika hilo la OECD. Uchunguzi uliofanywa chini ya msingi "ukosefu wa mapato sawa licha ya kukua kwa uchumi" unabainisha tofauti katika mapato ambayo kwa muda mrefu kwa mlingano na nchi za OECD ulikuwa mdogo sana ,sasa umekaribia kufikia kipimo cha OECD.Sababu iliopelekea hali hii,ripoti inasema, ni kupanda mno kwa mapato ya baadhi ya watu tangu kuingia karne mpya.

Ni nchini Ufaransa,Spian,Ireland,Ugiriki na Uturuki, ndiko mwanya kati ya masikini na matajiri kati ya 1985 na 2005 umepungua kidogo. Sababu kuu ya hali hii ya kuzidi ufukara shirika la OECD limeigundua ipo katika jamii zilivyo nchini Ujerumani.Koo zenye jamaa wachache zinahitaji pato la juu kwa kila mtu kuliko koo zenye jamaa wengi ili kuseleleza hali za maisha.

Ujerumani idadi ya wanaoishi pekee yao bila ndoa-singles au wanaoishi peke yao nje ya ukoo imeongezeka mno mnamo miaka michache iliopita na ukubwa wa ukoo wa wastani ni mdogo kuliko nchi nyengine zote isipokua Sweden-amesema bingwa wa OECD Michael Forster.Serikali ya Ujerumani kwahivyo, imetakiwa kurekebisha hali hiyo.

Ripoti ya OECD imegundua wanaoathirika mno katika hali hii ya ufukara ni watoto.Takriban katika nchi zote za shirika la OECD mzigo wa umasikini mnamo miaka 2 iliopita wazee wameuhamishia kwa watoto wao.Mtindo huu umetia fora zaidi Ujerumani.

Kiwango cha umasikini katika kundi la wakaazi wenye umri wa miaka 65 katika kipindi cha 1995 hadi 2005 kilisalia imara katika 9% wakati upande wa watoto katika muda huo hio ,kiliongezeka kutoka 11 na kufikia 16%.

Nchini Ujerumani ukosefu wa kazi umeongoza zaidi kuliko katika nchi yoyote ya OECD kuzidisha mwanya wa mapato usio wa haki.Pekee kutoka 1995 hadi 2005, mchango wa watu waliokaa katika nyumba ya wasio na kazi ilipanda kutoka kima cha 15.2 na kufikia 19.4%.Hicho ni kima cha juu kabisa kwa ujerumani ukilinganisha na nchi nyengine za OECD.