1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya shirika la biashara la kimataifa

Oumilkher Hamidou24 Machi 2009

Makadirio ya biashara ya nje si ya kuridhisha linasema shirika la WTO

https://p.dw.com/p/HIk8
Mwenyekiti wa shirika la biashara la kimataifa Pascal Lamy(kulia)Picha: AP


Shirika la biashara la kimataifa-WTO linakadiria shughuli za kibiashara ulimwenguni zitapungua kwa kadiri asili mia tisaa mwaka huu.Hali hiyo haijawahi kushuhudiwa tangu mwaka 1945,linasema shirika la WTO katika ripoti yake.


Shirika la fedha la kimataifa IMF liliashiria upungufu wa asili mia mbili wa biashara ya kimataifa,katika ripoti yake iliyochapishwa january mwaka huu.


Ripoti ya shirika la kimataifa la biashara WTO  itachapishwa kimsingi kesho,lakini vyombo kadhaa vya habari vimeshaitangaza ripoti hiyo tangu jana.


Kiwango cha biashara ya nje ya mataifa yaliyoendelea kitapungua kwa asili mia 10 mwaka huu,katika wakati ambapo kile cha nchi zinazoinukia kitapungua kwa asili mia mbili hadi tatu.


Ukuaji wa biashara ya kimataifa ulianza kudorora kwa ghafla mnamo nusu ya pili ya mwaka jana,pakishuhudiwa ukuaji wa kiuchumi wa asili mia mbili tuu kwa mwaka mzima,ukilinganishwa na ukuaji wa kiuchumi wa asilimia 6 kwa mwaka 2007-linasema shirika hilo la biashara la kimataifa WTO.


Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la kimataifa Pascal Lamy anahisi shughuli za biadhaa kadhaa za viwandani zimesambaa katika ulimwengu mzima ndio maana matokeo yake ni kupungua kiwango cha mahitaji.

Katika hali kama hiyo,mitindo ya kujipendelea inaongezeka na inatishia kuikaba biashara ya kimataifa,ambayo ni mojawapo ya mihimili ya ukuaji wa kiuchumi-amesema bwana Pascal Lamy.


Zikitathminiwa kwa sarafu ya Marekani ya dola,kiwango cha bidhaa za kimataifa zinazosafirishwa nchi za nje kimeongezeka kwa asili mia 15 mwaka jana na kufikia dala bilioni 15.800,katika wakati ambapo huduma zimeongezeka kwa asili mia 11 na kufikia dala bilioni 3.700.


Ujerumani kwa mara nyengine tena ndio iliyoongoza biashara ya nje mwaka jana kwa kusafirisha bidhaa zenye thamani ya dala bilioni 1.470,ikiitanagulia jamhuri ya watu wa China iliyosafirisha bidhaa zenye thamani ya dala bilioni 1.430.


Hata hivyo kwa mwaka huu wa 2009 makadirio si ya kuvutia anasema Anton Börner,mwenyekiti wa shirikisho la biashara jumla,biashara ya nje na huduma za jamii-BGA.


"Tunakadiria biashara ya nje kwa mwaka 2009 itapungua kwa asili mia 15 na biashara tunayoagizia kutoka nje itapungua kwa asili mia nane.Kwa hivyo tutakua na upungufu wa karibu yuro bilioni 846."


Shirika la biashara la kimataifa limewatolea mwito pia viongozi wa mataifa tajiri kiviwanda na yale yanayoinukia G-20 waahidi kuchukua hatua dhidi ya mitindo ya kujipendelea,wakati wa mkutano wao wa kilele April 2 ijayo mjini London.