1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya Usalama Munich

20 Februari 2017

Ripoti ya  mkutano wa usalama wakimataifa mjini Munich, inaelezea changamoto zasera za usalama duniani. Mada zinazozungumziwa katika ripoti hiyo ni pamoja na mpango wa kimataifa  dhidi ya ugaidi.

https://p.dw.com/p/2XiN6
Bilder von Wolgang Ischinger
Wolfang Ischinger Mkuu wa Mkutano wa Usalama wa MunichPicha: Bahri Cani

 Ripoti hiyo pia imekusanya habari juu ya vitisho vya wapiganaji wa jihadi, upoteshaji wa habari na pia utumiaji wa habari kama silaha pamoja na  hali ya usalama katika  eneo la bahari ya Pasifiki na mashariki ya kati. 

 Wolfgang Ischinger, mkuu wa mkutano wa kimatifa wa usalama duniani,ameandika kuwa usalama duniani kwa sasa ni tete ukilinganishwa na wakati wowote ule  tangu kumaliza kwa vita vikuu vya pili vya dunia, na vile vile tokea kumalizika kwa ukoloni wa nchi za magharibi na kutawala kwa siasa za kiliberali katika mfumo wa amani duniani. Sababu za kusema hayo ni pamoja na odhaifu uliopo katika umoja wa ulaya,usambazaji wa habari na pia uteuliwa wa Trump kuwa rais mpya wa Marekani.

München - Vorbereitung für die Sicherheitskonferenz
Maandalizi ya mkutano wa usalama wa MunichPicha: picture-alliance/dpa/Sputnik/G. Sisoev

Juu ya hayo pia kuna mjadala wa habari bandia na habari potofu, ambazo sasa zimekuwa pia changamoto katika uandikaji na uenezaji wa habari.

Changamoto zinazoikabili dunia katika maswala ya usalama

Hofu katika jamii zilizowazii hazianzi  kutoka ndani peke yake, bali pia zinaanza na habari zisizoridhisha  ambazo husambaa ndani ya jamii yenyewe.

Lakini changamoto kubwa katika usalama wa kimataifa, lipo katika makundi ya jihadi, yenye wafuasi pia katika nchi za magharibi. Wafanya mashambulizi Ulaya, wengine hutumia jina la jihadi kufanya  mashambulizi hayo. Nchi za ulaya pia hutafautiana  katika jinsi ya wanavyokabiliana na vikundi  vya ugaidi. Kwa mfano Ufaransa wao, walitangaza kuwa nchi yao iko katika hali ya  dharura, na huku Ujarumani hutumia njia ya kuvamia makaazi ya washambulizi na sehemu nyengine.

München - Vorbereitung für die Sicherheitskonferenz
Maandalizi ya mkutano wa usalama 2017 MunichPicha: picture-alliance/dpa/Sputnik/G. Sisoev

Kurasa 90 za repoti  ya mkutano wa  Munich wa  usalama  duniani, inatupa mtazamo, wa matatizo ya kisiasa ya dunia. Mwandishi wa ripoti hiyo ameandika  undani wa mikakati ya muelekeo utakaoweza kuumaliza mfumo wa dunia uliowekwa baada ya vita vikuu vya pili vya dunia na ambao unaweza kuathirika kwa kuzuka siasa kali za kizalendo katika bara la Ulaya.

Kwa sasa kunaoneka kuna udhaifu katika ushirikiano baina ya nchi kadhaa pamoja na kuweko kwa  migogoro baina ya nchi  mbali mbali.

Muandishi: Najma Said

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman